The House of Favourite Newspapers

Brazil Habari ni Nyingine, Yaitungua Mexico 2-0 (Video + Picha)

TIMU ya taifa ya Brazil imeendelea kuchakaza kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuiangamiza Mexico na kuiondoa katika michuano hiyo nchini Urusi kwa kuifunga mabao 2-0.

Neymar Jr ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia Brazil kunako dakika ya 51 ya mchezo huo.

Robeto Firmino aliiandikia Brazil bao la pili dakika ya 88 na kuihakikishia timu huyo kutinga robo fainali.

Timu zote mbili zilimaliza dakika 45 za kwanza bila yoyote kutikisha nyavu lakini mnamo kipindi cha pili Brazil walirejea vizuri na kuweza kuandika mabao hayo yote mawili.

Neymar anafikisha bao lake la pili katika michuano hiyo huku akiwa chachu ya ushindi katika kila mchezo timu yake inapokuwa uwanjani.

Brazil sasa watakutana na Ubelgiji ambao walitinga robo fainali kwa kuifunga Japan kwa bao 3-2.

Brazil (4-3-3):

Alisson 7; Fagner 5.5, T Silva 6, Miranda 6, Luis 6; Coutinho 6.5 (Firmino 86), Casemiro 6, Paulinho 6 (Fernandinho 81 7) ; Neymar 8, Jesus 7.5, Willian 8.5 (Marquinhos 91)

Manager: Tite 7

Goals: Neymar (51), Firmino (88) 

Mexico (4-3-3):

Ochoa 7.5; Alvarez 5 (Dos Santos 55), Ayela, Salcedo, Gallardo; Herrera, Marquez 5 (Layun 46), Guardado 7.5; Vela 7.5, Hernandez 5.5 (Kiminez 60), Lozano

Manager: J Carlos Osorio 6.5

Referee: G Rocchi (Italy) 7

Attendance: 41,970

 

Na Edwin Lindege | Global Publishers.

 

VIDEO: Neymar vs Mexico

Comments are closed.