The House of Favourite Newspapers

Nilisema Wabunge 17 wa CCM Mtwara na Lindi Bora Waondoke Tu!- Video

RAIS Dkt. John Magufuli amesema hafurahishwi na vitendo vya baadhiu ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuigeuka Serikali na kuanza kuishambulia Bungeni badala ya kutetea Ilani ya chama hicho kwa manufaa ya wananchi wao.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Julai 02, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha viongozi aliyowateua jana Jumapili kuziba nafasi za viongozi wengine aliyowaengua na waliostaafu na kusema kuwa ilifika wakati akamwambia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa ni bora wabunge 17 wa CCM mikoa ya Mtwara na Lindi waliokuwa wakipiga kelele Bungeni kuhusu sakata la Korosho wangeondoka kwenye chama hicho ili kuipisha Serikali iendelee kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.

 

“Nakupongeza Naibu Waziri wa Kilimo (Omary Mgumba) kwa kazi uliofanya Bungeni, huwa nafuatilia michango ya CCM, mwingine anasema tukienda hivi tutashindwa, kwa nini bado uko CCM, si utoke huko? Ulinyimwa nafasi ya kutetea hoja yako, mmoja akapewa nafasi ya kukupiga na mwingine tena akakupiga, hiki ulichokipata ndicho ulistahili, nakuomba ukashirikiane na wenzako Wizara ya Kilimo.

 

“Baadhi ya Wabunge wa CCM wanajisahau kuwa wanatakiwa kujibu kwa kuitetea Ilani ya CCM, lakini wapo wanaojisahau, mimi nafuatilia mijadala ya Bunge na ninaona. Watu wanashangilia uongo, tumechoka. Nilimpigia simu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa usiku, nikamuuliza kuna wabunge wangapi wa CCM, Mtwara na Lindi, akasema wapo 17, nikasema bora waondoke wote, hata Waziri Mkuu ni wa huko naye angeondoka, bado tutaweza kuongoza nchi.

 

“Ndiyo maana siku ya kupitisha bajeti nikamwambia Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru nenda Bungeni ukaangalie wabunhge wangapi wa CCM hawapo bungeni uwalime barua, na kweli amewaandikia barua wote,” alisema Magufuli.

 

Na Edwin Lindege | Global Publishers.

VIDEO: FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA

 

Comments are closed.