The House of Favourite Newspapers

Ubelgiji Yaiangamiza Japan Dakika za Nyongeza – Video + Pichaz

TIMU ya Taifa ya Ubelgiji imeipa kichapo Japan na kuiondosha katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kuitungua bao 3-2 na kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.

 

Ubelgiji waliutawala mpira katika takribani kipindi chote cha kwanza huku kukiwa na mashambulizi kwa timu zote mbili lakini hadi mapumziko wote walikuwa hawajafungana.

 

Kipindi cha pili upepo ulibadilika kwa Ubelgiji baada ya kudungwa bao la kwanza na Japa kupitia kwa Haraguchi dakika 48, dakika nne baadaye wakachapwa tena bao la pili kupitia kwa Inui dakika ya 52. Ubelgiji walitoka mchezoni, kwani walipoteza concentration na Japan wakatawala mpira kwa kiwango kikubwa huku wakikosa mabao mengine ya wazi.

Roberto Martinez alilazimika kufanya mabadiliko na kumtoa Yannick Ferreira-Carrasco huku nafasi yake ikichukuliwa na Nacer Chadli na Dries Mertens ikichukuliwa na Marouane Fellaini, mabadiliko yaliyoipa uhai Ubelgiji.

Dakika ya 69, Jan Vertonghen akaiandikia Ubelgiji bao la kwanza na Marouane Fellaini akifungika bao la kusawadhisha kunako dakika ya 74 kabla ya Nacer Chadli kukata mzizi wa fitina kwa kufunga bao la ushindi dakiza za nyongeza (90+4).

Ubelgiji sasa wanaendeleza ubabe na timu kutoka Bara za Asia kwenye mashindani hayo ambapo wamekutana nazo mara saba tangu mashindano ya Kombe la Dunia yaanze, ameshinda mara 4, droo 2 na kufungwa mara 1. Ubelgiji sasa watakipiga na Brazil kwenye mchezo wa robio Fainali ya kombe hilo.

BELGIUM: (3-4-3) Courtois 6; Alderweireld 6, Kompany 6, Vertonghen 7; Meunier 7, De Bruyne 7, Witsel 6, Carrasco 5 (Chadli 65 8); Mertens 6 (Fellaini 65 8), Lukaku 7, Hazard 8

SUBS NOT USED: Casteels (GK), Mignolet (GK); Batshuayi, Boyata, Dembele, Dendoncker, Hazard, Januzaj, Tielemans, Vermaelen

GOALS: Vertonghen (69); Fellaini (74); Chadli (94)

BOOKINGS: None

COACH: Roberto Martinez

JAPAN: (4-2-3-1) Kawashima 6; H. Sakai 6, Yoshida 7, Shoji 7, Nagatomo 7; Hasebe 6, Shibasaki 7 (Yamaguchi 81 6); Haraguchi 8 (Honda 81 6), Kagawa 7, Inui 8; Osako 6

SUBS NOT USED: Higashiguchi (GK), Nakamura (GK); Endo, Makino, Muto, Okazaki, Oshima, G. Sakai, Ueda, Usami

GOALS: Haraguchi (48); Inui (52)

BOOKINGS: Shibasaki (40)

COACH: Akira Nishino

REFEREE: Malang Diedhiou (Senegal)

MAN OF THE MATCH: Eden Hazard

VENUE: Rostov Arena

ATTENDANCE: 41,466.

Na Edwin Lindege

Belgium vs Japan 3 2 Highlights 2018

Comments are closed.