The House of Favourite Newspapers

BRAZIL: WATU 34 WAMEFARIKI BAADA YA BWAWA KUPASUA KINGO ZAKE


Watu 200 hawajulikani waliko baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil.

Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyikazi wa shirika hilo.

Shughuli ya kuwatafuta manusura inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika jimbo la Minas Gerais.


Gavana wa eneo la Minas Gerais Romeu Zema amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa matumaini ya kuwapata manusura ni madogo sana na huenda tu wakaishia kuipata miili.

Rais wa Brazil Jair Bolosonaro ambaye kufuatia mkasa huo alirudi nchini mwake kutoka kwenye Jukwaa la Kiuchumi Duniani nchini Uswisi, analitembelea eneo la mkasa huo pamoja na waziri wake wa ulinzi.

Baadhi ya watu waliyokwama kwenye matope, waliokolewa kwa kutumia helikopta baada ya barabara kuharibiwa.

Watu wengine wamehamishiwa kutoka makaazi yao kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Vale, Fabio Schvartsman thuluthi moja ya wafanyikazi karibu 300 hawajulikani waliko.

“Nina hofu nataka kujua hali ni mbaya kiasi gani” alisema Helton Pereira mmoja wa jamaa za watu waliyoathiriwa na mkasa huo aliyezungumza na BBC nje ya hospitali ya Belo Horizonte.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.