Breaking: Ajali ya Basi, Gari Dogo, Pikipiki Yaua Wawili Shinyanga

WATU wawili wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea mapema leo Jumatatu, Januari 13, 2020, asubuhi mkoani Shinyanga, ikihusisha basi la abiria la Kampuni ya Bright lenye namba T 437 DFJ lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dodoma na gari ndogo lenye namba T 173 ANW.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Isela, kata ya Samuye Shinyanga vijijini, Barabara ya Shinyanga – Tinde baada ya kugongana na gari hilo dogo na pikipiki (Bodaboda) wakati dereva wa basi akijaribu kumkwepa dereva wa pikipiki.

Polisi mkoani Shinyanga imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva Bodaboda na abiria wake walikuwa bado wamelaliwa na basi hilo huku juhudi za uokoaji zikifanyika haraka kunusuru maisha yao.

 

Toa comment