The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Chadema Waibuka na Daftari la Wapiga Kura – VIDEO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kulifanyika maboresho daftari la kudumu wapiga kura mapema ili kuepuka zima moto wakati wa hatua za mwisho za uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 24, 2018, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye mbele ya wanahabari ambapo amedai kuwa kazi hiyo ifanyike kwa muda muafaka na mapema ili baadaye isije kufanyika kwa dharura.

“Ikumbukwe kuwa, tangu uchaguzi mkuu ufanyike mwaka 2015, ni muda mrefu umepita, kuna watu wamekuwa na sifa za kupiga kura, tunaomba kazi hii ya kuboresha daftari kwa kuwaingiza ifanyike mapema,” amesema Sumaye.

“Mwakani kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matumizi ya rasilimali yatakuwa makubwa hivyo basi maboresho yafanyike mapema watu wapate uwezo wa kupiga kura,’’ amesema Sumaye.

VIDEO: Msikie Hapa Sumaye Akifunguka

Comments are closed.