JPM Amkabidhi Simbachawene Mikoba ya Lugola, Zungu Aula – Video

Rais Dkt. John Magufuli leo Januari 23, 2020 amemteuwa Mbunge wa Ilala Dar es salaam, Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene.

Rais pia amemteuwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Simbachawene anachukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo Januari 23, 2020 na Rais Magufuli kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na utendaji kazi katika Wizara hiyo.

Rais Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Hassan Zungu aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Aidha Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi leo Jenerali Kingu alikuwa Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani mpaka jana Januari 22,2020 ambapo aliandika barua ya kujuizulu nafasi hiyo na Rais akakubali ombi lake.

 

Rais Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu, Meja Jenerali Jacob Kingu, Kamishina Jenerali wa Magereza Faustine Kasike na Dkt.John Steven Simbachawene ambao vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye.

 

Rais Magufuli  amewaongezea muda wa miaka miwili Mabalozi saba; George Madafa (Italy), George Masima (Israel), Emmanuel Nchimbi (Brazil), Asha-Rose Migiro (Uingereza), Benedict Mashiba (Malawi) & Silvester Mabumba (Comoro) na DR Congo.
Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Thobias Andengenye na nafasi yake itajazwa hapo baadaye.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Rais Magufuli ameagiza TAKUKURU kuchunguza mkataba kati ya Kampuni ya nje ya nchi na Jeshi la zimamoto na uokoaji unaoelezwa kusainiwa kinyume cha sheria. Mkataba huo unatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Trillioni 1.


Loading...

Toa comment