The House of Favourite Newspapers

Breaking: Kisa Tundu Lissu, Kubenea Ajitoa Kugombea Chadema

0

KAMATI  ya Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo Jumatatu, Desemba 16, 2019, imetangaza majina ya waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

 

Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Desemba 18, 2019, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ameandika barua ya kujitoa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara na kusema kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu anafaa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kuliko yeye.

 

 

Chama hicho kimempitisha Mwenyekiti wa sasa, Freema Mbowe kugombea tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho Taifa huku Tundu Lissu akipitishwa kuwania nafasi ya Umakamu Mwenyekiti Bara. 

 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply