The House of Favourite Newspapers

Breaking: Mdee Huru Madai ya Lugha Chafu Dhidi ya Rais

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuacha huru Mbunge wa Viti Maalumu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Halima Mdee, baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo.

 

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Februari 25, 2021, na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yake.

 

“Baada ya kupitia ushahidi, nimejitosheleza upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka, hivyo mshtakiwa ameachwa huru,” amesema  Simba.

 

Mdee alidaiwa kutenda kosa hilo Julai 3, 2017, akiwa Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 

Kwa mara kwanza Mdee alipandishwa kizimbani  katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 10, 2017.

 

Alidaiwa kutenda kosa hilo wakati akiwa katika mkutano wake na waandishi wa habari   makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alidaiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais  John  Magufuli.

STORI NA DENIS MTIMA | GPL

Leave A Reply