The House of Favourite Newspapers

Mwendesha Mashtaka Anaswa Na Takukuru Akipokea Rushwa

0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Manyara imemkamata Mwendesha Mashitaka Mkoa wa Manyara, Mutalemwa Kishenyi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 5.

 

Kamanda wa Takukuru  Mkoa wa Manyara, Holle Makungu amesema Wakili  Kishenyi alikamatwa  Aprili 23, 2021 usiku akiwa anapokea  fedha hizo kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai ambao walikuwa wakikabiliwa na kosa la kukamatwa na risasi 370 na ‘sticker’ bandia zenye thamani ya shilingi bilioni 6.

 

Kamanda Makungu amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Leave A Reply