The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: AJALI YA TRENI DAR YAJERUHI WATU 9

TRENI ya abiria inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu, jijini Dar es Salaam imepata ajali baada ya mabehewa yake mawili kuanguka eneo la Karakata wilayani Ilala na kujeruhi watu 9, leo asubuhi, Ijumaa, Novemba 2, 2018.

Kamanda wa Reli nchini, David Mnyambuga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mabehewa hayo mawili yameharibika vibaya na kwamba majeruhi tayari walikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Endelea kufuatilia #GlobalHabariUpdates kwa habari zaidi.

UPDATES: Shirika la Reli Tanzania (TRL) limeanza kufanya utaratibu wa kuyainua mabehewa mawili ya treni ya Mwakyembe yaliyoanguka asubuhi ya leo katika eneo la Karakata, Ilala jijini Dar es Salaam ili kurejesha usafiri wa treni hiyo katika hali ya kawaida.

BABU WA GAMBA: “Bora ningekufa mimi, Isaac nilimuandikia urithi”

Comments are closed.