The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Bavicha Wahoji Kwa nini Chadema Pekee wanakamatwa?

0

Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), wamehoji sababu ya polisi kuwakamata wafuasi na viongozi wa CHADEMA pekee!

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrobas Katambi, amesema ameamua kuwaeleza Watanzania kuhusu mambo yanayotokea na hatua walizochukua ikiwemo kumuandikia barua IGP dhidi ya ukamataji unaoendelea. Akitetea hoja yake, alieleza sheria inaruhusu kufichua maovu pale yanapoonekana.

 

Katambi amelituhumu jeshi la polisi kwa kuwaandama wapinzani ilhali kuwa mpinzani si kosa kisheria. Amelalamikia suala la askari na viongozi wakubwa wa Serikali kuwanyanyasa watu na kusingizia kwamba kila wanachofanya ni agizo kutoka juu.

 

“Kwa nini wasio na hatia wanakamatwa na wenye hatia wanaachiwa huru?” alihoji Katambi.

 

Mwisho, amelitaka jeshi la polisi lisiwachukulie wapinzani kama maadui, bali liwaone kama watu wanaoelekeza utendaji mzuri wa serikali.

Leave A Reply