The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Bwege, Maharagande Wafikishwa Mahakamani

VIONGOZI wa ngazi ya juu wa Chama Cha Wananchi (CUF), ambao ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara maarufu kwa jina la Bwege, Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi, Mbarala Maharagande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Fatuma Karambwe na Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka,  leo wamefikishwa mahakamani mkoani Lindi kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili baada ya kushikiliwa tangu juzi Jumanne.

 

Bwege, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa katika eneo hilo, alikamatwa na wenzake hao, muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kata ya Kivinje, wilayani Kilwa juzi Novemba 20, 2018 na kupelekwa kituo cha polisi ambapo walinyimwa dhamana.

 

Uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kivinje, unafanyika kufuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Jafari Arobaini, kuamua kujiuzulu mwezi mmoja uliyopita kwa kile alichokiita, “kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kuiletea Tanzania maendeleo.”

 

Bwege amekuwa mmoja wa wabunge wanaojenga hoja za nguvu zinazoikosoa Serikali bungeni kuhusu kukithiri kwa mambo kadhaa, yakiwamo “mauaji, utekaji na utesaji” bila wahusika kukamatwa wala kuchukuliwa hatua.

 

UPDATES:

Mahakama imewapa dhamana Mbunge Suleiman (Bwege), Mbarala Maharagande na Abuu Mjaka kwa masharti ya mdhamini 1 kwa kila mshtakiwa na dhamana ya maandishi ya Tsh. 1m. Kwa hoja kuwa majina yamekosewa kwenye fomu, Polisi wamesema muda umekwisha na hivyo wamerudishwa rumande wasubiri kesho asubuhi.

AJIUA KIKATILI KISA PENZI LA BINAMU YAKE – VIDEO

Comments are closed.