The House of Favourite Newspapers

Breaking: Magufuli Ashinda Urais, Kura Mil. 12.5 – Video

0

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Dkt. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 12,516,252 kati ya kura 15,091,950 zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

 

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuwa, Dkt. Magufuli ndiye mgombea aliyepata idadi kubwa zaidi ya kura kuliko wagombea wengine 14 huku mpinzani wake mkuu, Tundu Lissu wa Chadema akiachwa mbali zaidi na kuwa wa pili kwa kupata jumla ya kura 1,933,271.

 

Walioandikishwa kupiga kura – 29,754,699
Waliopiga kura – 15,091,950
Kura halali – 14,830,195
Kura zilizokataliwa – 261,755.

 

Matokeo

Dkt. John Magufuli (CCM) – 12,516,252
Leopold Mahona (NRA) – 80,787
John Shibuda (ADA Tadea) – 33,086
Mutamwega Mgaywa (SAU) – 14,922
Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini) – 14,556
Yeremia Maganja (NCCR) – 19,969
Prof. Ibrahim Lipumba (CUF) – 72,885
Philip Fumbo (DP) – 8,283
Bernard Membe (ACT) – 81,129
Queen Sendiga (ADC) – 7,627
Twalib Kadege (UPDP) – 6,194
Hashim Rungwe (Chauma) – 32,878
Mohammed Mazrui (UMD) – 3,721
Seif Maalim Seif (AFP) – 4,635
Tundu Lissu (Chadema) – 1,933,271.

 

Aidha, Jaji Kaijage amesema kuwa, Jumapili, Novemba 1, 2020, mshindi wa Urais, Dkt. Magufuli atakabidhiwa hati ushindi wa urais na ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi la uchaguzi na matokeo, na kitakachofuata ni kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mhula mpya.

 

Leave A Reply