The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mahakama Kenya Yaidhinishwa Ushindi wa Kenyatta (Video)

0

Ekuru Aukot: Tumefurahishwa na uamuzi wa Mahakama

Mmoja wa waliogombea urais nchini Kenya, Ekuru Aukot,  amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ambayo alisema imedhihirisha uhuru wake na kujitolea kwake kudumisha sheria.

Amesema: “Wanasiasa hawawezi kuwa majaji na mahakimu.”

” (Majaji wa Mahakama ya Juu) Walifanya hivyo 1 Septemba walipofuta ushindi wa Kenyatta, na wamerudia tena leo,” amesema.

“Tunatumai kwamba sasa Kenya inaweza kusonga mbele, na wanaochochea ghasia kutokana na mzozo wa uchaguzi sasa hakuna mzozo tena baada ya uamuzi wa mahakama.  Tunaweza sasa kuangazia mambo ya uzito zaidi. Chama chetu (Thirdway Alliance) sasa kutaangazia kuhakikisha Serikali inafanya kazi ipasavyo.”

 

Duale: Wakati umefika kwa Wakenya kusonga mbele

Kiongozi wa wengi katika Bunge la Taifa, Aden Duale, amesema wakati umefika sasa kwa Wakenya kusonga mbele.

Amesema Wakenya sasa wanafaa kuangazia kuungana pamoja, na amesema kuna njia nyingi za kuendeleza umoja.

“Wakenya walipiga kura na kumchangua Kenyatta, ushindi wake ulipingwa tena na leo tuna furaha kwamba kwa kufuata sheria, ushindi wa Kenyatta sasa umeidhinishwa kwa kauli moja,” amesema.

 

Maraga: Majaji wameamua kesi zote hazina msingi

Jaji Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.

Kesi ya Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.

Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake.

Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21.

Leave A Reply