The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mama Mzazi wa Erick Kabendera Afariki Dunia

0

MAMA mzazi wa mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera, Bi Verdiana Mjwahuzi, amefariki leo Desemba 31, 2019 nyumbani kwake Chang’ombe jijini Dar es Salaam na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana.

 

Desemba 13, mwaka huu, mama huyo alizungumza na waandishi wa habari akimuomba Rais John Magufuli amsamehe mwanaye kwani ndiye aliyekuwa akimtegemea kwa kila jambo zikiwepo gharama za matibabu yake.

 

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la ukwepaji wa kodi, kuongoza genge la uhalifu  na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 170, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda kati ya Januari 2015 na Julai 2019, maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

 

Leave A Reply