The House of Favourite Newspapers

Breaking News: CCM Yatangaza Majina ya Wagombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

DAR ES SALAAM: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina 12 ya makada wake ambao watawania kuteuliwa ili waweze kuwa wawakilishi kwenye Bunge la Afriika Mashariki (EALA).

Akitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa, miongoni mwa waliyoteuliwa; makada 8 ni kutoka Tanzania Bara na 4 kutoka Zanzibar.

“Katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa chama kwenye uteuzi wa wabunge wa EALA, tulitoa matangazo, tukapata wana CCM 450 walioomba kupewa ridhaa hiyo ya kuiwakilisha nchi kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Miongoni mwao wanawake ni 93 na wanaume ni 357 ambao wote walipita kwenye michujo tukapata majina haya 12.”

“Mchakato unaofuata ni kuyapeleka majina haya 12 Bungeni Dodoma ili yakapewe ridhaa na bunge, watakaoshinda ndiyo watakuwa wawakilishi wetu EALA.”

“Chama kinawapongeza wale wote waliopata uteuzi na ambao wamekosa, tuendelee kushikamana na kukijenga chama chetu pamoja na nchi yetu.” Alisema Polepole.

Waliopata uteuzi

Bara

Wanawake

  1. Zainab Rashid Mfaume Kawawa
  2. Happiness Elias Lugiko
  3. Fancy Haji Nkuhi
  4. Happiness Mgalula

Wanaume

  1. Dkt. Ngwalu Jumanne Maghembe
  2. Adam Omary Kimbisa
  3. Isey Macha
  4. Charles Makongoro Nyerere

Zanzibar

Wanawake

  1. Mariam Yusi Yahya
  2. Rabia Abdallah Hamid

Wanaume

  1. Abdallah Hasnu Makame
  2. Mohammed Yusuf Nuhu

TAZAMA VIDEO YA POLEPOLE AKITANGAZA MAJINA HAYO

Comments are closed.