The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: RAPA NIPSEY AUAWA KWA RISASI

RAPA

wa Marekani, Nipsey Hussle (33) ameuawa kwa kupigwa risasi, asubuhi ya kuamkia leo, Aprili 1, 2019, jijini Los Angeles nchini humo.

 

Inasemekana Hussle, alimiminiwa risasi akiwa nje ya duka lake la nguo na kwamba katika tukio hilo watu wengine wawili walijeruhiwa pia kwa kupigwa na risasi.  Polisi wamesema hakuna taarifa zozote za mshukiwa kwa wakati huu na bado wanaendelea kufanya uchunguzi.

 

 

Picha ya mwisho ya Rapa Nipsey Hustle akiwa nje ya eneo la tukio na tweet ya mwisho aliyoiandika.

 

Nipsey ameacha watoto wawili (Kross na Emanuel) na ‘girlfriend’ wake Lauren London. Rapa Nipsey atasikika ndani ya album mpya ya DJ Khaled ambayo inategemewa kuingia sokoni Mei 17.

 

Baadhi ya mastaa walioomboleza kifo cha rapa huyo kupitia mitandao yao ya kijamii,

 

Comments are closed.