The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Tundu Lissu Akamatwa na Polisi Mahakamani Kisutu

MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amekamatwa na Jeshi la Polisi, leo Machi 6, asubuhi katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Lissu aliyekuwa amekwenda mahakamani hapo kusikiliza kesi yake nyingine ya uchochezi, amekamatwa nje ya mahakama hiyo mara baada ya kumaliza kusikiliza kesi hiyo.

Global Publishers imefanikiwa kuzungumza na Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene, ambaye amethibitishwa kukamatwa kwa Lissu.

“Ni kweli Tundu Lissu amekamatwa alipokuwa akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake. Polisi hawajaeleza kwa nini wamemkamata na huenda wamempeleka kwa Kamanda Simon Sirro kuhojiwa, hatuna taarifa zaidi tutawajuza,” alisema Makene.

Mtandao wa Global Publishers umefanya jitihada za kumtafuta Tundu Lissu kwa njia ya simu ambaye amekiri kukamatwa na jeshi hilo.

“Nimekamatwa na polisi, wamenileta hapa sentro lakini mpaka sasa hawajaniambia kosa langu ni lililosababisha wanikamate,” alisema Lissu.

Tunaedelea kufuatilia, tutawajuza kila linaloendelea kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu.

Comments are closed.