The House of Favourite Newspapers

Chadema: Lissu Amevunjwa Mguu na Nyonga Lakini Jasiri, Tumuobee!

0
Viongozi mbalimbali wa Chadema.

CHAMA cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kimesema hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye alishambuliwa na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita na sasa anatibiwa katika Hospitali jijini Nairobi, Kenya, haijatengemaa kwani bado anaendelea kufanyiwa upasuaji ulioathiri sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo miguu, nyonga na mikono.

Viongozi mbalimbali wa Kamati Kuu ya Chadema wamesema hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi yao iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ambapo waliwaomba wananchi kuchangia chochote katika kuokoa uhai wa mbunge huyo.

Katika mkutano huohuo, viongozi hao walieleza kutokuwa na imani na jeshi la polisi na serikali katika kuwatafuta na kuwabaini waliokula njama za kumshambulia mbunge huyo.

Leave A Reply