Breaking: Tetemeko la Ardhi Lapiga Dar & Pwani


TTEMEKO la ardhi lenye kipimo cha richter 5.9, limepita katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania na kudumu kwa sekunde kadhaa, hasa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya Mkoa wa Pwani likizua taharuki kubwa kwa wananchi.

 

Tetemeko hilo limepita katika maeneo ya Mikocheni, Sinza, Temeke, Manzese, Ilala, Tabata, Gongo la Mboto, Ubungo na maeneo mengine majira ya saa 2:14 usiku wakuamkia  leo, Jumatano, Agosti 12, 2020.

Maeneo mengine ambayo yamepitiwa na tetemeko hilo kwa Mkoa wa Pwani ni Kibiti, Mkuranga, Vikindu na maeneo ya karibu na hayo.

Hakuna madhara yaliyoripotiwa kutokana na tetemeko hilo lakini limezua taharuki kubwa na hofu.

Tunaendelea kuwapa taarifa kuhusu tukio hilo,  endelea kufuatilia mitandao yetu.
Toa comment