The House of Favourite Newspapers

Wananchi wa Jimbo la Buchosa Kuanza Kilimo Cha Parachichi

0
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo akiwa kwenye mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kijiji cha Iseng’he Kata ya Luharanyonga.
Wananchi wa Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wanatarajiwa kuanza kilimo cha  zao la parachichi kutokana na mazingira ya eneo hilo kuwa na mvua nyingi na ardhi yenye rutuba ya kustawisha zao hilo.
Buchosa ni kati ya halmashauri saba zinazounda mkoa wa mwanza lakini ni eneo pekee katika mkoa wa mwanza linalopata mvua mwaka mzima hivyo kufanya mazao ya aina mbalimbali kustawi katika eneo hilo.
 Mbunge wa Jimbo hilo Eric Shigongo akiwa kwenye mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kijiji cha Iseng’he Kata ya Luharanyonga amewaeleza wananchi wa jimboni hilo kuwa zao la parachichi ni miongoni mwa mazao ambayo yanafaida kubwa hivyo ni vyema kuanza kilimo cha zao hilo.
Shigongo amesema wananchi wa buchosa wamejikita kulima zao la miti ya mbao kama zao la kiashara ambalo linachukuwa muda mrefu wa miaka 20 hadi 30 ili kufikia kiwango cha kuvuna lakini zao la parachichi ni kati ya miaka mitatu hadi minne tu na kuanza kuvuna.
Mazao mengine ya chakula na biashara yanayolimwa kwa wingi katika Jimbo la buchosa ni mpunga ,mahindi,viazi na mihogo hivyo likiongezeka zao la parachichi litakuwa  zao la kiashara la  muda wake mfupi kuanza kupata faida.
Shigongo amesema hali ya hewa ya Buchosa inafafana na hali iliyoko mkoa wa Njombe unaolima za la parachichi kwa wingi  hivyo tulikubaliana na kamati ya fedha na mipango ya halmashauri yetu kuanza kilima hiki cha zao la parachichi na tutaanza kugawa  mbegu siku sio nyingi ili wananchi wetu weweze kunufaika na kuondoa umasikini kwenye jamii ya wanabuchosa.
“Tutaweka utaratibu madhubuti ya kupata Miche hiyo ya parachichi kupitia Halmashauri yetu na wananchi wataendelea kununua hapa kwa bei nafuu”amesema Shigongo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Luharanyonga Hezeron Samike amewaomba wananchi wa Buchosa kuchangamkia fursa hiyo ambayo itakuwa mkombizi kwa wakulima wa kata hiyo na Jimbo black buchosa kwa ujumla.
Mmoja wananchi wa Kijiji cha Iseng’he John Malima amesema kuanzishwa kwa kilimo cha zao hilo kitaisaidia wananchi kupata manufaa Kwa haraka kutokana na kupata mavuno mapema.

Leave A Reply