The House of Favourite Newspapers

BUNGE LIVE: Mkutano wa 11 Kikao cha Sita – VIDEO

Kikao cha sita mkutano wa 11 Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari kimeanza Bungeni Dodoma, wabunge wameanza na maswali na majibu kwa wizara mbali mbali.

 

Serikali imedhamiria kuweka kipaumbele cha kujenga nyumba za walimu za kuweza kuishi familia moja hadi 6 kwa gharama nafuu, ili kuondoa tatizo la ukosefu wa nyumba za walimu nchini.

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda amesema serikali inatumbua upo uhaba mkubwa wa nyumba za walimu kwa shule za msingi na sekondari ndio maana imekuwa ikijitahidi kila mwaka kujenga nyumba za walimu.

 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewaomba wabunge wasaidie kuwahimiza waganga wa mikoa, wilaya kuhakikisha wanaagiza dawa na vifaa vinavyo husiana na suala la uzazi wa mpango ili ziweze kuwasaidia wananchi.

 

“Serikali katika mwaka huu wa fedha 2018/19 tumeweza kuongeza bajeti ya mpango wa afya ya uzazi kutoka Bil. 5 hadi Bil. 18. Mwanamke kupata ugonjwa wa festula maana yake ni kwamba hakupata huduma nzuri wakati alipokuwa anakaribia kujifungua, kwasababu festula haipaswi kutokea kama mwanamke alipata huduma nzuri ya uangalizi wakati anajifungua,” Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Ndugulile.

 

“Kila taifa lina utamaduni wake na lazima liulinde kwa udi na uvumba, tunachokifanya sisi sio kwamba tuna vita na wasanii wetu, lengo letu ni kulinda maadili ambayo katika kipindi hiki cha utandawazi kumekuwepo na mmong’onyoko mkubwa na lazima tuchukue hatua,” Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Mwakyembe.

Comments are closed.