The House of Favourite Newspapers

Askofu Gwajima Apewa Akutwa na Hatia ‘Asimamishwe’ – Video

0

Kamati ya Bunge imetoa azimio sakata la Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kupewa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge.

 

Akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka Bungeni amesema;

 

“Kamati imebaini kauli za Mhe. Gwajima zinadhalilisha nafasi ya Mbunge na kushusha heshima ya Bunge, wabunge na viongozi, zinachonganisha mhimili wa bunge dhidi ya Serikali na wananchi, zinaonyesha dharau na kushusha heshima ya bunge na uongozi wa Bunge.” Mwakasaka, M/Kiti Kamati

 

MAONI YA KAMATI YA BUNGE

“1. Vyombo vya kisheria vifuatilie mwenendo na vitendo vya Askofu Josephat Mathias Gwajima kutokana na kauli mbalimbali alizotoa kwa vina ashiria kuwepo na jinai na uvunjifu wa amani na usalama wan chi.

 

“2. Suala hili lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria na maadili ya umma, lifikishwe kwenye chama anachotoka, ili aweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni za chama chake,” amesema Mwakasaka.

 

MAAZIMIO YA BUNGE

“Bunge linaazimia kwamba, Mhe. Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe apewe adhabu ya kutohudhuria Mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitishwa ka azimio hili.” – Emmanuel Mwakasaka, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati Gwajima alifanya makosa hayo kati ya tarehe zifuatazo; 25 Julai, 01 Agosti  15 Agosti, 21 Agosti.

 

Leave A Reply