The House of Favourite Newspapers

Busungu aleta tafrani, awaondoa watatu Yanga

0

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Deus Kaseke (kulia) Godfrey Mwashiuya (kushoto) na Donald Ngoma,Dhidi ya KMKM kwenye mchezo wa Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.Yanga ilishinda mabao 2-0.(Picha na Yusuf Badi)

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
KUINGIA kwenye kikosi cha kwanza cha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu, kumewapa wakati mgumu viungo wa pembeni, Mbrazili, Andrey Coutinho, Geofrey Mwashiuya na Simon Msuva.

Awali, Busungu alikuwa akianzia benchi kwenye kikosi cha Mholanzi huyo ili kuwapisha, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwenye nafasi kabla ya kuhamishiwa pembeni kucheza kama kiungo mshambuliaji.
Busungu alianza kuaminika na kuanza kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza cha Pluijm wakati timu hiyo ilipovaana na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara akitokea benchi kuchukua nafasi ya Msuva na kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 huku lingine likifungwa na Ngoma.
Tangu siku hiyo, mshambuliaji huyo alikuwa akipangwa kucheza kiungo wa pembeni kama siyo namba 7 iliyokuwa inachezwa na Msuva, basi 11 waliyokuwa wanapokezana Coutinho na Mwashiuya.
Wakati Busungu akicheza nafasi moja ya kiungo wa pembeni, nafasi nyingine ya pembeni wamekuwa wakipangwa Haruna Niyonzima au Salum Telela.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Pluijm alisema amelazimika kumpunguza kiungo mmoja na kumuanzisha Busungu kwa ajili ya kuiongezea kasi safu yake ya ushambuliaji namba 9 na 11 zinazochezwa na Ngoma na Tambwe.
“Bidii, kujituma kwake na nidhamu kubwa anayokuwanayo ndani ya uwanja, ndiyo imenilazimu nimuanzishe kwenye kikosi changu kwanza, kwa sababu anacheza kwa kufuata maelekezo yangu.
“Kingine zaidi uwezo wake wa kupiga mashuti na jinsi anavyopambana na mabeki wa timu pinzani, hivyo sioni sababu ya kumuweka benchi na badala yake ataanza kikosini kwangu,” alisema Pluijm.

Leave A Reply