The House of Favourite Newspapers

Cannavaro, Kessy Wasimulia Kilichowaua

0
Nahodha Mkuu wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam, Championi Jumatatu
NAHODHA Mkuu wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na beki wa pembeni wa timu hiyo, Hassan Kessy wametaja kilichowaondoa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Hayo, waliyasema mara baada ya mechi ya marudiano iliyochezwa juzi na kupokea kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya MC Alger ya nchini Algeria, hivyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-1.
Championi Jumatatu, Cannavaro alisema: “Waarabu mara zote tunazokutana nao wanatutoa nyumbani kwao na kikubwa ni fitna pekee za ndani na nje ya uwanja na siyo kitu kingine.
“Wale waamuzi ndiyo waliotuua kiukweli, kwani alikuwa akipuliza filimbi kwenye mipira ya kugombea na wachezaji wa Alger walikuwa wanajidondosha kisha faulo kuelekezwa kwetu,” alisema Cannavaro.


Kwa upande wa Kessy alisema: “Hakuna asiyejua fitna za timu za Kiarabu, kwenye mechi hii iliyomalizika muda siyo mrefu niseme waamuzi ndiyo wamewabeba, kwani waamuzi walikuwa upande wao kwa sababu maamuzi yao hayakuwa sahihi na kujikuta tukipoteza, lakini tumejifunza.”

SHOO YA HARMORAPA, JUMA NATURE, MSAGA SUMU, DULA MAKABILA DAR LIVE

Leave A Reply