The House of Favourite Newspapers

Carina Ashindwa Kutoka katika Hospital ya Rufaa ya Bugando Kisa Deni

0

UPDATES; Deni la shilingi milioni tatu, limemfanya msanii wa Bongo Muvi, Carina kushindwa kutoka katika Hospital ya Rufaa ya Bugando, baada ya kutokuwa na fedha ya kulipa deni lililotokana na gharama za matibabu hospitalini hapo alipotibiwa kwa zaidi ya mwezi sasa.

Akizungumza na Global TV, Carina alisema mwanzo walikuwa wakidaiwa shilingi milioni nane, ambayo walichangachanga familia wakalipa, lakini bado likabaki deni hilo, ambalo linamfanya azidi kusota hospitalini hapo.

“Nimekaa muda mrefu sana hospitalini nazidi kusikia vibaya bora nitoke tu nirudi nyumbani maana nimeshachoka kabisa na sijisikii vizuri tena,” alisema Carina kwa maumivu makali.

Mwigizaji wa Bongo Muvi ambaye kwa takribani miaka sita sasa ni mgonjwa wa tumbo baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara 21 na sasa akiwa amefanyiwa upasuaji wa 22 katika Hospitali ya Bugando Mwanza, anapopatiwa matibabu kwa sasa, ameomba kama kuna mtu yeyote aliwahi kumkosea ambaye ndiye anayesababisha ateseka basi amsamehe.

Akizungumza na mwandishi wa Global TV, @imeldamtema hospitalini hapo, Carina amefunguka mengi ya kuumiza jinsi anavyoteseka.

Carina ambaye hivi sasa anadaiwa bili ya hospitali ya kiasi cha shilingi milioni tano ili aweze kutoka hospitalini hapo baada ya kukaa kwa zaidi ya mwezi mmoja akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa hospitalini hapo akiwa hajitambui, ameomba Watanzania waendelee kumsaidia kwa hali na mali.

Kama utapenda kumsaidia Carina namba za kumchangia hizi hapa chini.

0769990045 M-PESA Carolinhawa Hussein Ebrahim bounin

0789095858
Fatuma Maruzuku

Akaunti: 0152591586500 (Carolinhawa Hussein)

Leave A Reply