The House of Favourite Newspapers

Rais wa Zanzibar Dk. Mwinyi Amshukuru Rais Dkt. Samia

0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega tangu Mzee Mwinyi alipoanza kuugua mwezi Novemba alipopelekwa Uingereza kwa matibabu.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Machi 3, 2024  katika hitma na Dua Maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ilyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tarehe 3 Machi 2024.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amewashukuru pia Madaktari wa Hospitali ya Mzena kwa kazi kubwa waliyoifanya kujaribu kuokoa maisha ya Mzee Mwinyi pamoja na Masheikh, Waalimu, Ndugu, Marafiki na wananchi kwa dua nyingi walizomuombea Mzee Mwinyi kwa kupindi chote alichokuwa akiugua na baada ya kufariki.

Leave A Reply