Kartra

Cavani Amuachia Jezi Ronaldo

Klabu ya Manchester United imemkabidhi rasmi jezi namba 7 kwa Cristiano Ronaldo ambaye amesajiliwa hivi karibuni.

Namba 7 ilikuwa inavaliwa na mshambuliaji Edison Cavani ambaye amepewa namba 21 ambayo awali ilikuwa inavaliwa na Daniel James ambaye ameuzwa kwenda Leeds United.

Ronaldo amemshukuru Cavani kwa kukubali kumpa jezi hiyo ambayo ina historia kubwa kwa mchezaji huyo.

‘Sikutarajia kuwa itawezekana kuvaa tena namba 7, Namshukuru sana Cavani kwa ukaribisho huu murua”


Toa comment