The House of Favourite Newspapers

CCM Yaitisha Kikao cha Dharura Dodoma, Maombolezo Siku 21 – Video

0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza siku 21 za maombolezo kwa wanachama wa chama hicho kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ambaye pia alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifariki dunia jana Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

 

 

Tangazo hilo limetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania, Humphrey Polepole wakati akizungumza na wanahabari katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Taifa jijiji Dodoma.

 

 

 

“Ninawaletea taarifa ya msiba baada ya wakuu wa chama chetu kupokea tarifa rasmi, wakuu wa chama wametafakari baada ya hapo tunatoa taarifa ifuatayo;

 

 

“CCM kinatoa taarifa rasmi ya kifo cha Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. CCM tumepikea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Dkt. Magufuli.

 

 

“Taarifa ya serikali iliyotolewa na Makamu wa Rais, Mama Samia ilieleza kuwa ndugu Magufuli amefariki kwa tatizo la moyo, kitaalam cardio fibrillation. Wakuu wa chama waliopo wameshauriana na kukubaliana kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa itaketi Jumamosi, Machi 20, 2021 ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar.

 

 

“Chama kitakuwa katika maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo za seerikali, bendera za chama zitapepea nusu mlingoti, kutakuwa na vitabu vya maombolezo bara na Zanzibar.

 

 

“Chama kinawaomba wananchama wote wa CCM na watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu kuwa na kuendelea kuwa watulivu huku tukitafakari mchango wa kipekee na kihistioria wa ndugu yetu ndugu Magufuli,” amesema Polepole.

 

Leave A Reply