The House of Favourite Newspapers

Chadema Yataka Kuonana na Rais Samia

0

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeomba kuonana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali utakaoliletea taifa furaha, haki na ustawi.

 

 

Akizungumza na vyombo vya habari jana Jumapili, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema amemuandikai barua Rais Samia kumuomba kuonana naye;

 

 

“Wote tumejifunza, serikali ikiharibikiwa, nchi yote inaingia simanzi. Hii haina maana sisi wa Chadema tumegeuka waimba mapambio wa Rais Mama Samia. Inatupa sisi changamoto ya kuongeza juhudi za kuboresha sera zetu na kuongeza ushindani wa hoja.”

 

 

Bw Mbowe amesema wanategemea kumweleza Mama Samia na kumkabidhi mapendekezo yao kadhaa ya kina ya namna bora ya kuanza upya katika azma ya “kujenga utengemano wa nchi” na akaongeza kuwa wanaamini atatambua nafasi ya vyama vya upinzani.

 

 

“Hatupaswi kumtakia mabaya kwa sababu tu ni zao la CCM. Bali tunatakiwa kuongeza juhudi na maarifa kumkabili kwa ushindani wenye kujenga na siyo kubomoa. Tunamwombea afanye mema wakati wa utawala wake ili kupata ustawi wa taifa letu.”

 

 

Mbowe amesema kuwa: “kauli za rais, Mama Samia Suluhu Hassan zinatuchanganya na anapaswa kulijua hili. Anapoongea nia yake ya kuenzi sera, mipango na tabia ya Magufuli, taifa linasinyaa na kuhuzunika.”

Leave A Reply