The House of Favourite Newspapers

Chanzo hasa cha upungufu wa nguvu za kiume-2

0

Couple-in-BedUpungufu wa nguvu za kiume siyo ugonjwa ila ni dalili ambayo ndani yake inaweza kuwa na magonjwa mengi au sababu tofauti. Tatizo hili limegawanyika katika makundi matatu, kwanza ni sababu za kisaikolojia.

Mtu mwenye tatizo linalotokana na sababu hii hushindwa kufanya tendo la kujamiiana wakati siku chache zilizopita aliweza, hulalamika anakuwa na hisia zote na uume kusimama lakini anapohitaji hushindwa. Mwili unakuwa vizuri lakini uume unalegea ghafla hata akilazimisha hawezi, mwingine hulalamika kushindwa alipozoea lakini akienda kwa mwingine hulifanya tendo hilo kwa ufanisi.

Tatizo hili huweza kumtokea mtu kama hakuna maelewano mazuri na mwenza wake, mazingira ya tendo siyo mazuri au kuna tatizo kikazi, kimasomo au hakuna maelewano mazuri. Endapo kuna hali kama hii basi inabidi ichunguzwe vizuri ili hatua makini ichukuliwe, uchovu wa akili pia huchangia.

Tatizo hili kisaikolojia likiendelea huathiri mfumo mzima wa mwili na kusababisha tatizo kuwa kubwa na kuingia katika sababu ya pili ya kifioziolojia.

Katika chanzo hiki cha pili cha hali au sababu ya kifiziolojia ‘Physiological Factors’ mwanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kabisa na kikamilifu. Tatizo hili hutokana na hali ya mwili kushindwa kufanya kazi ya kuamsha na kuuendesha uume, hapo sababu inaweza kuwa upungufu wa virutubisho muhimu mwilini, upungufu wa vichocheo, tatizo la kisaikolojia kwa ujumla wake, mwili kuchoka. Kwa hiyo katika tatizo hili tunasema ni jinsi mwili unavyofanya kazi.

Tatizo hilo huchunguzwa hospitali kwa kupimwa vipimo mbalimbali ili kuhakikisha mwili upo vizuri kama presha, sukari, damu, kuangalia vichocheo na vingine ambavyo daktari ataona inafaa.

Tatizo hili la kifiziolojia husumbua sana na likiendelea hufikia katika hatua ya tatu ambayo ni kubwa.

Mwanaume aliye katika hatua hii pamoja na kushindwa kusimamisha uume, pia hupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Uume hushindwa kusimama, hata akijaribu aidha anashindwa, huweza kufanikiwa kupenya ukeni lakini huwa hauna nguvu na kujikuta mara kwa mara anawahi kumaliza tendo. Wakati mwingine hata kuingiza ukeni hadi kuusaidia kwa nguvu kidogo.

Mwanaume mwenye tatizo hili hata anapomaliza tendo, manii zinapotoka, baada ya hapo huchoka sana au huhisi mwili unauma kwa kukosa stamina, kushindwa kuendelea na tendo la pili, humtokea hata yule wa tatizo la kisaikolojia.

Sababu ya tatu ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo la kiugonjwa au patholojia. Hapa mwanaume anakuwa na tatizo kubwa la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume kutokana na tatizo endelevu la kifiziolojia, magonjwa sugu mwilini au homa kali au maumivu makali ya sehemu za mwili. Pia matumizi ya baadhi ya dawa za magonjwa sugu mfano ya presha, moyo, sukari, kansa, HIV, na mengineyo huchangia.

 Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply