The House of Favourite Newspapers

Udongo kaburi la Kanumba wauzwa mamilioni ya fedha

0

KanumbaMAYASA MARIWATA, amani

DAR ES SALAAM: Maajabu! Baada ya Gazeti la Risasi Mchanganyiko wiki iliyopita kuandika habari yenye kichwa; KABURI LA KANUMBA LAVUNJWA, hatimaye waliofanya uharibifu huo wamejulikana, AMANI limeambiwa.

Katika habari hiyo, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Steven Charles Kanumba ambaye sasa ni marehemu, lilivunjwa na kuchotwa udongo na mchanga upande wa miguu na kichwani mwa kaburi, hali iliyozua sintofahamu kwa wanafamilia, akiwemo mama wa marehemu, Flora Mtegoa.

kaburi la kanumba labomolewa (1)UCHUNGUZI WA AMANI

Katika uchunguzi wake, Amani lilibaini kuwa, waliohusika na uchukuaji wa udongo na mchanga huo ni baadhi ya wafanyabiashara wa Kikongo ambao walitumia kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000) kufanikisha tukio hilo.

Jumanne iliyopita, gazeti hili lilifika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar na kukutana na baadhi ya watu wanaosimamia makaburi hayo ambao walisema kuwa wana wasiwasi na watu wanaofanya biashara kwamba, walichukua kwa lengo la kusaka utajiri kwa kutwaa nyota ya marehemu Kanumba.

“Unajua Kanumba alikuwa supastaa mkubwa hapa Bongo. Sasa nina wasiwasi waliochukua udongo na mchanga ule, walitaka kuwa na nyota kwenye biashara zao kama Kanumba,” alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.

kaburi la kanumba labomolewa (5)CHANZO KUTOKA KWA MAMA KANUMBA

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mama wa staa huyo, mara baada ya taarifa za kaburi hilo kuvunjwa kuripotiwa gazetini, kuna mtu alimpigia simu mama huyo na kumwambia kuna wasanii wa Kongo walimuomba awasaidie kupata udongo na mchanga wa kaburi la marehemu huyo.

“Yaani ilivyotoka ile habari kwenye gazeti lenu tu, kuna mtu alimpigia simu mama na kumwambia alitamani kumpa ishu hiyo kipindi kirefu lakini alikuwa akiogopa na hakujua jinsi ya kumpata, lakini alivyoona habari ndipo akapata ujasiri.

kaburi la kanumba labomolewa (6)“Alisema kuna Wakongo walimuomba afanye juu chini kuwasaidia wapate udongo kidogo tu wa kaburi hilo kwa upande wa kichwani na miguuni kwa lengo la kusafisha nyota zao kisanii na walikuwa tayari kumlipa kiwango chochote cha fedha lakini akawakatalia kutokana na hofu licha ya kumuahidi watahakikisha jambo hilo halijulikani,” alisema mtu huyo.

Akaongeza: “Walimuahidi kuwa watanunua udongo huo kwa shilingi milioni kumi bila kuweka deni. Inaonekana hao Wakongo wanajua huu mchezo wa kuvuta nyota za marehemu waliokwi-shazikwa, maana kutoa milioni kumi kununua udongo tu si mchezo.”

MAMA KANUMBA ATAFUTWA

Baada ya kuunasa ubuyu huo, gazeti hili lilimsaka mama Kanumba ili kumuuliza ukweli wa madai hayo ambapo alikiri kupokea simu nyingi zikimueleza mambo ya namna hiyo, ila bado inamuwia vigumu kujua undani wa ishu hiyo iliyotawaliwa na ushirikina kwani haamini kama mtu anaweza kufanikiwa kwa njia hiyo.

“Nimeshangaa sana maana nilipata simu kama mbili tofauti, kuna watu walinieleza kwamba kuna wasanii wa nje walikuwa wakihaha kusaka udongo wa kaburi hilo, nilidhani haya mambo ni hapa nyumbani tu kumbe hata hao wasanii wa nje wana imani potofu kiasi hicho! Imenisi-kitisha sana japo hatujui kama ndiyo hao waliofanya tukio hilo au la ila namwachia Mungu,” alisema mama Kanumba.

Aliongeza kuwa, miongoni mwa watu hao waliompigia simu, yupo aliyemwambia kuwa wamekuwa wakinunua udongo wa makaburi ya marehemu wenye majina makubwa kwa bei kubwa, kuanzia kiasi cha shilingi milioni kumi na kuendelea bila kujali.

Leave A Reply