The House of Favourite Newspapers

Chongolo Atoa Miezi Minne kwa Wakandarasi wa REA Kufikisha Umeme Vijijini

0

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametoa miezi minne kwa wakandarasi wote walioingia mikataba na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kufikia April 30, 2023 kila kijiji katika Mkoa wa Morogoro umeme uwe umewaka.

 

Aidha amemtaka Waziri wa Nishati, January Makamba apite kila kijiji kuwasha umeme na CCM itashuhudia zoezi hilo la uwashaji kwa kuwa wananchi hawataki kusikia lolote zaidi ya kupata umeme.

 

“Nimeongea na Waziri wa Nishati, January Makamba amenihakikishia kuwa umeme utawaka kila kijiji, sasa ole wake mkandarasi atakayakwenda kinyume na maagizo haya ataona, haiwezeni Mheshimiwa Rais ametoa fedha tayari na zipo kwenye akaunti za watu wanashindwa kuwajibika ipasavyo kwa uzembe,” amesema Chongolo.

 

Mkoa wa Morogoro una wilaya saba na halmashauri tisa ambapo Wilaya ya Kilosa na Mvomelo mpaka sasa bado kuna idadi kubwa ya vijiji ambavyo bado havina umeme.

Leave A Reply