Vigogo Chama cha Walimu (CWT) Wamegomea Uteuzi wa Rais Samia?
Siku chache zilizopita, Rais Samia Suluhu Hassan, aliwateua viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kuwa miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya.
Rais wa CWT, Leah Ulaya yeye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Geita wakati Katibu Mkuu wa CWT, Japhet Maganga yeye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa.
Leo, Januari 30, 2023 ndiyo siku ambayo walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wameripoti kwenye vituo vyao na kuapishwa na wakuu wao wa mikoa.
Hata hivyo, gumzo kubwa ni kwa viongozi hao wa CWT ambapo wakati wenzao wakiapishwa, wao wameonekana mkoani Tanga, kwenye kikao cha viongozi wa juu wa CWT, jambo lililoibua maswali mengi kuwa ni je, wamegomea uteuzi wa Rais Samia?
Mkutano huo umefanyiwa katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga na inaelezwa kwamba wawili hao, kwa nyakati tofauti, walionekana wakihojiwa na maafisa wa Jeshi la Polisi.