The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-26

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
“Mambo?” Musa alisalimia.

“Poa tu,” mama Shua alijibu kwa mkato sana huku akichukua tahadhari kwa lolote endapo mumewe angetokea na kuhisi vibaya.

Akili haikumpa mama Shua, akaamua kumpigia simu baba Shua lengo ni kutaka kujua aliko lakini simu yake iliita kwa muda mrefu sana bila kupokelewa.
JIACHIE MWENYEWE…

Baba Shua aliiona simu hiyo ya mkewe lakini hakuona sababu ya kuipokea…
“Kwanza niipokee ili iweje? Najua anataka kujua kuhusu nilipo, halafu akishajua ili iwe nini? Mbona mimi sitaki kujua mambo yake?” alisema moyoni baba Shua na ili kupangua simu ya mkewe, alimpiga mabusu Maua mpaka wakajikuta wakiangukia kwenye kochi kubwa…puu..!

Ukimya ulitawala, kilichosikika ni miguno ya mmmmm…mmmm, Maua alikuwa akihema kwa nguvu kama aliyetoka kufukuzwa…
“Mmmm…mmmm…”

“Ngoja nikafunge mlango,” alisema Maua, baba Shua akamwachia kwa muda.
Maua alifunga mlango haraka na kumrejea baba Shua pale kwenye kochi kubwa. Ukimya ukaendelea kutawala lakini mihemko ya hapa na pale ilisikika kiasi kwamba, kama chumbani kungekuwa na mtu mzima anafuatilia, lazima angetoka kuungana na wawili hao…

“Benny,” aliita Maua kwa sauti iliyotoka kwa chini sana…
“Yes Maua,” Benny naye aliitika kwa kufuata biti ya kuita ya Maua…
“Si utachelewa kazini wewe?”

“Hata kama…usijali Maua.”
Maua kusikia hivyo, akamshika mkono wa kulia baba Shua na kusimama naye, wakaenda chumbani, wakajifungia na kupanda kitandani..!

Figisufigisu ilitawala kitandani, Maua alikuwa akionesha umahiri kwenye uwanja kwa mkakati wa kumrejesha baba Shua kwenye himaya yake. Muda mwingi wa mchezo alimtaka asahau machungu ya kwa mkewe, kwani yeye yupo kwa ajili yake.
***
Baada ya nusu saa, Maua alikuwa amemshika mkono baba Shua, wakawa wanatoka nje. Mkononi Maua alishika funguo za gari…

“Sasa baby si uende na gari…au utakuwa umesahau kuendesha?” alisema Maua…
“Nisahau kuendesha gari sweet..! Haitawezekana hata siku moja.”
Baba Shua alipokea funguo, akazama kwenye gari na kuondoka…

“Kishakwisha huyu…safari hii hachomoki! Ndiyo atajua mapenzi ya kweli yalikuwa wapi kati yangu na yule malaya wake wa nyumbani,” aliwaza Maua akiwa anarudi ndani.
Yeye ni mfanyabiashara wa kuuza nguo za kike na vipodozi toka nchini Thailand na shughuli zake ni popote. Wakati mwingine wateja wake hufika hadi nyumbani. Tena wengi ni wale wanaonunua kwake kwa jumla na kwenda kuuza rejareja madukani mwao.

Kuna siku Maua anaweza kushinda nyumbani na kujikuta akiingiza milioni mpaka kumi.
***
Mama Shua akili ilimlala kabisa. Hakuamini kama baba Shua anaweza kumchunia kiasi kile…
“Ana maana gani sasa kukaa kimya kiasi hiki? Mimi nifikirieje? Kama ameona mimi na yeye basi, si aseme tu kuliko kuwekana roho juu namna hii,” alisema moyoni mama Shua lakini sauti nyingine ilimjibu…

“Kwanza shukuru Mungu wewe…angekuwa mwanaume mwingine angekuua hata kwa kukuchinja! Wewe umeona wapi mume au mke anamwona mwenzake akiingia chumbani kwa mtu mwingine ili kusaliti halafu anavumilia tu?”
Mama Shua aliamua kuvaa, akaondoka. Lakini si kwenda kazini kwake, bali kwa baba Shua akajue nini kilimsibu.

Akiwa ameshatoka, mbele alimwona Musa akiingia kwenye gari lake, mama Shua akasimama mahali ili kumpa nafasi Musa ya kupotea kwanza mbele ya macho yake ndipo na yeye aendelee na safari yake.
Mama Shua anafika nje ya ofisi ya mume wake, baba Shua naye anawasili kwa gari la Maua.

Aliegesha gari mahali, akashuka na kutembea kwa mwendo wa pole kuelekea ndani. Mama Shua hakuweza kuvumilia na alijuwa kwa tabia ya mume wake ya siku mbili zile, angeweza kumpita bila kumsemesha, akasimama njiani kwenda ndani…

“Baba Shua nataka tuongee kidogo,” alisema mama Shua kwa sauti ya chini sana…
“Mimi na wewe tutaongea nini sasa? Na tangu lini mahali pa kuongelea pamekuwa hapa ofisini?” alijibu baba Shua akiwa anaendelea kutembea kiasi kwamba, baadhi ya wafanyakazi walipoiona picha hiyo walishangaa kwani wanawajua wawili hao kwamba ni mke na mume.

Mama Shua hakutaka makuu, akaamua kugeuza kuondoka huku moyoni akiwa na faraja kwani alishajua mumewe amefika kazini lakini alikuwa na maswali kibao…
“Hili gari ni la nani? Halafu kama jipya! Kalitoa wapi? Au huko alikokwenda? Maana kwa muda aliotokea nyumbani isingekuwa rahisi ndiyo awe anafika kazini muda huu, lazima alipitia mahali…

“Atakuwa amelinunua au kalikopa? Lakini lilishaanza kutembea,” aliwaza moyoni mama Shua akitokomea kabisa eneo hilo.
Alifika nyumbani akiwa amechoka sana kiakili na mwili. Aliwaza namna ya kuwasiliana na mama yake na kumweleza matatizo yake lakini moyo ulisita. Alijua ataamsha hasira za mama huyo.
Alimwangalia mtoto wake, Shua. Akamhurumia sana huku akitingisha kichwa.
***
Saa sita mchana, Musa alimtumia meseji mama Shua…
“Upo?”
Je, baada ya mama Shua kuiona meseji hiyo alifanyaje? Usikose kufuatilia katika Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu.

Leave A Reply