The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-29

0

ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:

Msichana wa kazi aligunia moyoni. Kwake lilikuwa tukio geni sana kumwona bosi wake akiingia chumbani kwake na mwanaume. Hajawahi kuona!

Simu ya baba Shua iliita, akaitupia macho na kuona jina la mke wake, akaipuuza…

“Baby mbona hupokei simu?” Maua alimuuliza…

SHUKA NAYO SASA…

 Ah! Si yule malaya anapiga…”

“Ungepokea sasa…unajua anataka kukwambia nini?”

“Achana naye,” alisema baba Shua akianza kukunja sura.

Maua baada ya kauli hiyo, hakutaka kupoteza muda, akapanda kitandani na kuanza kumvua nguo baba Shua huku tayari akiwa na mihemko ya kimahabamahaba…

“Baby,” aliita Maua kwa sauti yenye kuashiria kubembeleza mwana…

“Niambie Maua…”

“Nikupe dawa ya kumwacha mke wako?” aliuliza Maua kwa sauti iliyotoka nje kwa kupitia tundu za pua…

“Kama ipi Maua?”

“We sema uko tayari au hauko tayari?”

“Niko tayari…kwa mambo anayonifanyia? Aisee niko tayari…hivi hapa ninavyojua mimi kwa sababu ameshatekwa na huyo Musa wake hataweza kurudi kwenye reli ninayoitaka mimi kama mume.”

“Da! Aisee pole sana. Basi mimi nitakupa…lakini nikwambie mapema, hiyo dawa si ya mitishamba wala vidonge vya hospitali.”

“Ni dawa gani sasa jamani Maua mpenzi wangu, hebu niambie kidogo basi…”

“Wala usiwe na wasiwasi Benny kwani wewe si unahisi mkeo anakusaliti?”

“Maua si kwamba nahisi, ni kweli ananisaliti. Nimekwambia anaingia chumbani kwa mpangaji mwenzangu nikiwa namwona kwa macho yangu halafu unasema nahisi, maana yake nini? Halafu yule kijana tangu anahamia pale siku ya kwanza nilimuazia vibaya kwamba atakuwa ananisaliti na mke wangu, sijui kwa nini niliwaza hivyo?!”

“Huenda ni akili yako ilijiongeza tu. Wapo watu wameumbwa hivyo. Wanajiongeza wenyewe hivyo huwa hawahitaji kuongezwa.”

“Oke, sawa…sasa niambie hiyo dawa ni ipi?”

“Nitakwambia, we tuendelee kuwa pamoja tu,” alisema Maua huku akimshika mikono baba Shua na kuanza kumnyooshanyoosha. Pia akahamia sehemu mbalimbali za mwili na kumkandakanda huku akimpongeza kwa maneno ya mahaba…

“Benny…”

“Niambie Maua…”

“Unajua namshangaa sana huyo mke wako…”

“Kwa nini? Japokuwa hata mimi mwenyewe namshangaa…”

“Yaani mwanaume mzuri kama wewe anakutenda hivi?! anajua thamani ya mwanaume kweli? Tatizo binadamu wengi wanapenda kupata lakini hawawezi kutumia…

“Utakuta watu wanapishana kwenye maofisi kutafuta kazi lakini wakishapata hawatendi. Mimi huwa naamini watu wengi wanatafuta ajira na siyo kazi…”

“Una maanisha nini Maua kwa huo mfano wako?” aliuliza baba Shua…

“Namaanisha kwamba, siku hizi wanawake wengi wanatafuta kuolewa lakini si ndoa…”

“Ha! Maua, kuolewa na ndoa si jambo moja mpenzi wangu?”

“Hapana Benny! Kuolewa ni mwanamke kumpata mwanaume wa kuishi naye akahesabiwa yeye ni mke wa fulani. Ndoa ni zile taratibu zilizopo. Yaani uvumilivu, uaminifu na tendo lenyewe.

“Sasa kama mke anaingia kwenye chumba cha mwanaume ndani ya nyumba moja hiyohiyo, huyo anaijua ndoa kweli? Si alitafuta kuolewa tu!”

Benny alimwelewa vizuri Maua kiasi kwamba alimkisi kama ishara kwamba, amemkubali. Maua naye akambusu Benny, kisha wakazama kwenye tukio lingine la denda! Kwa dakika kadhaa hakuna aliyekuwa akiongea.

Kila mmoja aliguswa na hisia za mapenzi yao miaka miwili nyuma ambapo walikuwa moto.

Kutokana na hali hiyo, walifika mahali kila mmoja alifanya anachotaka kwa vitendo bila kutoa sauti.

Mfano, Maua alipotaka Benny ageuke alimshika na kumgeuza, Benny akajua na kuendelea kujigeuza mwenyewe.

Benny naye alipotaka Maua alale chali, alimshika akaashiria kumlaza, Maua akalala mwenyewe huku akiyakaza macho kwa mwelekeo wa mwanaume huyo kama anayeuliza ‘kuna lingine?’

Hali iliendelea hadi wakafika mahali wakajikuta tayari wapo uwanjani na mechi imeanza.

Siku hiyo, Maua alitumia ufundi wake wote kuhakikisha anakidhi hitaji la mapenzi kwa Benny. Ilifika mahali hata Benny mwenyewe alishangaa kuona mambo makubwa kwa Maua. Akajiuliza amepatia wapi uzoefu huo?

Kingine alichokifanya Maua siku hiyo ni kwenda sambamba na Benny huku akiendelea kumsifia kwa mambo mbalimbali, akikumbushia hata madogo tu aliyoyafanya Benny zamani kuhusu yeye.

Ukichanganya na sauti aliyokuwa akiitumia sasa, weee! Benny namaanisha baba Shua, alisahau kabisa kama alifunga ndoa na sasa ana mtoto mmoja wa kike anaitwa Shua.

Kichwani alianza kumsahau ghafla mama Shua. Ile hali ya kuumia moyo kwa sababu ya usaliti wake ilianza kumtoka na kujiona kama kawaida. Akili yake ya wivu ilianza kuhamia kwa demu wake huyo…

“Maua,” aliita huku mikiki ya mpira ikiwa inaendelea…

“Abee…”

“Unajua nikija kukuona na mwingine nitakasirika..?”

“Ukiniona na mwingine au na mwanaume mwingine? Maana unaweza kuniona nikiwa na shoga yangu Hadija, pia utakasirika sweet?” aliuliza Maua.

Hapo ni baada ya mechi yao kufika mwisho na sasa walikuwa wamepumzika huku wakihema kwa kasi ya shughuli pevu…

Je, kiliendelea nini? Usikose mwendelezo wake katika Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu.

Leave A Reply