The House of Favourite Newspapers

CORONA: Hospitali Ya Kanisa Yaanza Kutoa Matibabu Bure, Askofu Aeleza..

0
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Cente Dkt. Eliud Isangya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Kanisa la International Evangelism Cente lenye makao makuu yake eneo la Sakila Wilayani Arumeru mkoani Arusha,kupitia zahanati ya kanisa hilo limetangaza kutoa bure huduma ya matibabu kwa makundi maalum wakiwemo wanawake,wazee, watu wenye ulemavu na watoto chini ya umri wa miaka mitano lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na virusi vya corona vinavosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu.

Askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt. Eliud Isangya akizungumza na waandishi wa habari amesema kuanzia Aprili 29, 2020 zahanati hiyo haitatoza kiasi chochote cha fedha kwa makundi hayo endapo watafika kupata matibabu yote yanayotolewa hapo.

 

Amesema kama kanisa mbali na kutoa huduma za kiroho kwa waumini wake ambao wengi wapo maeneo ya vijijini, imeonelea ni vyema kutoa huduma hiyo bure baada ya kutambua mtikisiko mkubwa wa kiuchumi uliosababisha kuyumba kwa kipato cha nchi, mashirika, makampuni mbalimbali mpaka kwa wananchi mmoja mmoja.

Baadhi ya wananchi wanaopata huduma ya matibabu katika zahanati hiyo ya kanisa wameshukuru kauli hiyo ya kiongozi wa kiroho kwa kuona umuhimu kwa wananchi hususani katika kipindi hiki kigumu ambaacho upatikanaji wa fedha umekuwa mgumu hivyo wananchi nao wakatumia fursa hiyo kulishukuru kanisa kwa huduma hiyo ya bure kama.

Aidha askofu Isangya amesisitiza kuwa kanisa hilo litaendelea na maombi mbalimbali kwa ajili ya kuliombea taifa na viongozi wake ili nchi iwezo kuondokana na ugonjwa huo hatari unaotikisa dunia na kuharibu uchumi wa nchi na watu.

Leave A Reply