The House of Favourite Newspapers

CORONA: Mwigulu Awavaa Chadema kwa ‘Kutomwona’ Rais

0

 

BUNGE wa Iramba Magharibi (CCM) Mwigulu Nchemba, amewashambulia wabunge na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai yao kwamba hawamwoni Rais John Magufuli katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Covid-19, akiwaambia kwamba, “Rais siyo nesi, kwamba anapaswa kuwa mbele akiwa anahudumia wagonjwa.” 

 

Mwigulu ameyasema hayo wakati wa kujadili bajeti ya wizara ya afya bungeni jana Aprili 30, 2020, iliyowasilishwa na waziri mwenye dhamana, Ummy Mwalimu.

 

Wizara hiyo ilipata wachangiaji wengi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, ambao mpaka sasa umeshagharimu maisha ya Watanzania 16.

 

 

Leave A Reply