The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Kukondeana! Daktari Aliyemfanyia Wema Upasuaji Avunja Ukimya

0

Kwa siku za hivi karibuni stori zilizozagaa mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni juu afya ya msanii wa Bongo Muvi, Wema Sepetu kukondeana na kuwa na muonekano tofauti aliozoeleka machoni mwa jamii inayomzunguka.

 

Mrembo huyo ambaye nyota yake ilianza kung’aa na kujizolea umaarufu baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania 2006, kukondeana kwake kumezua mijadala mbalimbali huku baadhi yao wakisema amekatwa utumbo.

Kufuatia hali hiyo juzi mwanahabari wetu alikutana laivu na daktari aliyemfanyia Wema oparesheni ya kupunguza mwili.

 

Akizungumza na mwandishi wetu daktari huyo alianza kwa kujitambulisha kuwa Japhet Omondi ambaye alikuwa na haya ya kusema;

 

“Mimi natoka kwenye taasisi ya Viva Serenity yenye makao yake nchini Kenya ambapo tushughulika na masuala mbalimbali ya afya ikiwemo kupunguza mwili.

 

“Hivyo hata, Wema Sepetu naye alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kupunguza mwili wake na kutaka aonekane mwembamba na mimi ndiye niliyekabidhiwa jukumu hilo.

 

“Nilimfanyia vipimo vyote vya awali kama ilivyotakiwa ila oparesheni tulimpeleka nchini India ikiwa chini ya usimamizi wangu,” alisema Dokta Omondi.

 

Kufuatia kuzagaa taarifa za mrembo huyo kukatwa utumbo dokta Omondi alieleza ukweli kuhusu alichofanyiwa mrembo huyo;

 

“Tunaona mitandaoni kila mtu akiongea lake kuhusu afya ya mteja wetu lakini ukweli ninaokueleza ndugu mwandishi ni kwamba Wema hajakatwa utumbo isipokuwa tumeubana sehemu fulani ili usipitishe chakula kama ulivyokuwa ukipitisha awali na kumsababishia kunenepeana.

 

“Si kwamba tumemkata utumbo kama wengi wanavyofikiria na kusambaza maneno yasiyokuwa na ukweli, “ alisema.

Kuhusu kukondeana kupitiliza Dokta Omondi alisema hali hiyo haina madhara yeyote ya kiafya na yuko salama kabisa.

 

Mwanahabari alipomuuliza kama mrembo huyo anaweza kufanyiwa matibabu ya kurudia unene wake Dokta Omondi amesema halina shida kwakuwa utumbo wake tumeubana hivyo tunaweza kumfanyia oparesheni nyingine na kwenda kuuachia ingawa si mshauri kufanya hivyo kwa sasa,” alisema Dokta Omondi.

 

Wakati Dokta Omondi akihitimisha mahojiano na gazeti hili mrembo mwingine kutoka Nairobi nchini Kenya aliyejitambulisha kwa jina la Tajilaimana Mohammed amesema naye ni miongoni mwa waliofanyiwa mpango wa upasuaji na Viva Serenity kwa ajili ya kupunguza unene.

 

Tajilaimana amesema alikwenda kwenye taasisi hiyo akiwa na kilo 140 ambapo alifanyiwa upasuaji huo ambapo mwili wake ulipungua mpaka kilo 67 lakini aliona kama amekonda sana hivyo alifanya tena upasuaji kwa ajili ya kuongezeka mwili mpaka kilo 80 alizokuwa akizihitaji, alisema Tajilaimana.

 

Viva Serenity ni taasisi iliyoanzia nchini Kenya ambapo sasa imeingia hapa nchini kwa ajili ya kuwahudumia wanaotaka kupunguza miili yao ambapo Dokta Omondi amewaomba warembo vibonge wanaotaka kuwa mamondo wajitokeze kwenda kwenye taasisi hiyo ili iwahudumie.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Leave A Reply