The House of Favourite Newspapers

Dalali Kuchukua Kodi ya Mwezi ni Ujambazi

0

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amewapiga marufuku madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa wapangaji na badala yake pesa hizo walipwe na wenye nyumba.

 

Kauli hiyo ameitoa hii jana Novemba 15, 2021, mkoani Iringa na kusema kwamba kitendo cha kuchukua pesa kwa mtu anayepanga ni wizi wa waziwazi.

 

“Kuna baadhi ya madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa mpangaji kodi ya mwezi mmoja,mi sikujua kama kuna wizi wa namna hii, mimi nilikuwa najua wanalipwa na aliyemtuma…ni ujambazi kabisa…

 

“Hao madalali wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo, wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, mwenye nyumba lazima akulipe wewe…

 

“Marufuku kabisa kwa dalali kuchukua, kulazimisha anayepanga nyumba akulipe posho ya mwezi mmoja,” amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi.

Leave A Reply