The House of Favourite Newspapers

Darassa: Namheshimu Alikiba

0

RAPA Darassa amefunguka jinsi ambavyo wimbo wake #ProudofYou alioimba na Ali Kiba ulivyofanyika ambapo pia ameeleza kuwa wimbo huo ulikaa takribani mwaka mzima ndani bila kuuachia.

kwenye #PlanetBongo ya East Africa Radio #Darassa amesema; “Mimi huwa nakaa na nyimbo muda mrefu sana, #ali mwenye alikua anaona huyu jamaa ana matatizo gani.

“Nakumbuka nilikutana naye #Johannsburg akaniambia wamekuachia sasa umepata akili kwasababu ni ngoma kubwa na unajua #King amekuwa kwenye game kwa muda mrefu na heshima yake huwezi kuchezea.

“Wakati natoa #ilikeit #ProudofYou ilikua ndani tayari kama miezi sita, kwahiyo nafikiri ni wimbo ambao ilikua imepangwa aje anibless kipindi ambacho natoa album yangu.

“Na nafikiri ni wimbo kwa sasa huwezi kumpigia tena #King unataka kolabo acha kwanza #proudofyou ikae hapo so namuheshimu kwa hilo na alijitoa sana katika kuutengeneza huu wimbo,” amesema Darasa.

Leave A Reply