The House of Favourite Newspapers

DAWASCO Kuwatibu, Kuwalipa Fidia Waathirika wa Moto wa Gesi Buguruni

MAMLAKA ya maji safi na maji taka jiiji Dar Es Salaam imesema imepokea majeruhi watano waliounguzwa na moto uliosababishwa na kupasuka kwa bomba la gesi eneo la Buguruni kwa Mnyamani wakati mafundi wake wakifanya kazi.

Dawasco wamesema wamewahamishia wagonjwa hao hospitali ya Taifa ya Muhimbili na walichukua muda ili kuhakikisha majeruhi hao wanatokana na ajali ya moto huo.

DAWASCO itahudumia huduma zote kwa majeruhi hao mpaka watakapopata afya njema. Pia wamesema kitengo cha maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu kitafanya tathimini ili kujua ni namna gani watashirikiana na DAWASCO kulipa fidia waathirika wa kiuchumi.

Comments are closed.