The House of Favourite Newspapers

DC abembeleza penzi la Lungi, akataliwa

0

lungiStori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mmoja wa Wakuu wa Wilaya (DC) wa Kanda ya Ziwa ambaye pia ni kada kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwenye mbwembwe (jina linawekwa kwenye mabano kwa sasa), anadaiwa kutamani penzi la mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lungi Maulanga.

Habari zilizotua kwenye safu hii ya Ubuyu wa Vigogo zilieleza kuwa, mheshimiwa huyo alimuona Lungi kupitia kwa rafiki yake ambaye ni mbunge wa moja ya Majimbo ya Kanda ya Kati mwa nchi aliyekuwa mpenzi wa staa huyo.

Chanzo makini kililiambia Wikienda kuwa, bila kujali kuwa ni ‘shem’ wake DC huyo alianza kubembeleza penzi hasa kupitia mitandao ya kijamii huku akiomba iwe siri ili rafiki yake asimuone kuwa ni msaliti.

Hata hivyo, katika kuhofia jamaa huyo alitumwa na mbunge ili kumwona kama ni mwaminifu, Lungi alimkatalia lakini bado jamaa hajakata tamaa.

Gazeti hili lilimtafuta mkuu huyo wa wilaya lakini simu yake haikupatikana hewani hivyo jitihada zinaendelea ili naye aanikwe kwenye safu hii.

Kwa upande wake, Lungi alithibitisha mheshimiwa huyo kukosa usingizi juu ya penzi lake ilihali ni mume wa mtu mwenye familia na watoto wawili.

Je, una ubuyu wa kigogo yeyote? Wasiliana na safu hii kwa simu namba 0713 750 910

Leave A Reply