The House of Favourite Newspapers

DC JOKATE ATUA +255 GLOBAL RADIO, AIMWAGIA SIFA

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, Jokate Mwegelo akifanya mahojano na +255 Global Radio katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori, Dar,  Feb 26, 2019.

 

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefanya ziara katika Ofisi za Makampuni ya Global Group na kutoa pongezi za dhati kwa namna ilivyompa supoti katika kazi zake mbalimbali.

Meneja wa Vipindi wa Global Radio, Borry Baraka (aliyekaa) akifanya mahojiano na DC  Jokate Mwegelo.

Pia, DC Jokate amefurahishwa kwa kuanzishwa radio ya +255 Global Radio ikiwa na lengo la kumfikia kijana kisasa zaidi. Mkuu huyo wa wilaya alizungumzia pia mradi wa kuendeleza elimu wilayani kwake aliouita Tokomeza Ziro ambapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani atakuwa mgeni rasmi Machi 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar.

Kusikiliza +255 Global Radio => LISTEN LIVE

Borry Baraka akimuonesha kitu na DC Jokate Mwegelo. Wengine kutoka kushoto Mhariri Mwandamizi Elvan Stambuli na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.
DC Jokate Mwegelo (kola nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa +255 Global Radio baada ya mahojiano.
DC Jokate akiwa na Global Group, Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho.
DC Jokate akiwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.
Meneja Mkuu wa Global Group,  Abdallah Mrisho (kushoto) akimkaribisha DC Jokate  +255 Global Radio.
DC Jokate akisalimiana na wafanyakazi wa +255 Global Radio.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.