Dereva wa Lori Lililolipuka Ruvuma Apatikana, Amevunjika Mbavu!

DEREVA Hubert Mpete aliyekuwa akiendesha lori la mafuta lililopata ajali usiku wa kuamkia jana Mkoani Ruvuma, amepatikana akiwa hai.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (RPC), Simon Marwa,  amesema dereva huyo ana michubuko kidogo na amevunjika mbavu, hivyo wamempeleka hospitali kwa matibabu.

 

Marwa amesema uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo ingawa shehena ya mafuta lita 33,000 alizobeba zimekutwa salama na mmiliki wa mafuta hayo ameshayahamisha.

 

Lori hilo mali ya James Mwinuka ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Njombe Filling station lilipata ajali juzi Jumapili Agosti 11,2019,  saa 4 usiku baada ya kuacha njia na kugonga mti Kijiji cha Hangangadinda mkoani Ruvuma.

 

Scania hilo lenye namba ya usajili T 243 BCU, na tela T 685 DCV, liliungua kwa moto katika kijiji hicho, Halmashauri ya Madaba, Ruvuma,  ambapo kichwa chote cha lori kiliteketea kwa moto na kubakiza tenki pekee lililokuwa na lita 33, 000 za petroli.


Loading...

Toa comment