The House of Favourite Newspapers

Diamond aangua kilio ukumbini!

12

IMG_7514

Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akilia.

Musa mateja

SIYO sinema! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda, twende na Ijumaa Wikienda.

Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.
DAKIKA CHACHCE KABLA YA KULIAIMG_7504….Akibembelezwa.

Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya ambao ndiyo habari ya ‘mujini’ kwa sasa.

Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.

MASHABIKI WALICHANGIA?
Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

IMG_7500

Queen Darleen akimtoa kwenye steji.

DADA’KE AMTOA JUKWAANI
Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

NYUMA YA JUKWAA
Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

IMG_7497
AAA WAPI!
Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.

“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

IMG_7498Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!

SHOO IKAWA IMEISHA
Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.

SHABIKI ASIMULIA KUGUSWA KWAKE
Naye shabiki mmoja ambaye hakutaja jina, alizungumza na gazeti hili kufuatia Diamond kumaliza shoo kwa kulia:

“Dah! Nimeguswa na wimbo wa Diamond kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nimejikuta nikilia kama ilivyomtokea jamaa. Inaonekana anajua kutunga sana.
“Unajua kilichomfanya Diamond alie ni namna alivyowaona mashabiki wake wakihuzunika baada ya kuanza kuimba akapela yake.”

IMG_7499Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Diamond na kumuuliza kisa cha kulia vile ambapo alisema:

“Mwana ile hali huwa inatokea. Unajua wimbo wenyewe unanigusa mimi katika kila hatua. Nilijiuliza, iko siku nitakwenda Dar Live kuimba halafu nikakosa watu? Iko siku kumbe mimi nitakuwa si kitu tena, sitapendwa!”

12 Comments
  1. Glady Eugen says

    in evy step u made platinum you av tu pray

  2. Andrew says

    Usikitisha mziki huo unagusa mno i love u my plutnum

  3. Godwin malila says

    That its truth diamond

  4. key judge says

    Dah pole sana bt sjawahi skia hiyo song

  5. Edward Meshack says

    Unajua kaka Diamond ktk maisha kuna kupanda na kushuka ila namwomba Mungu aendelee kkn’garisha from Kigoma KASULU.

  6. Julian Juliasi Justine says

    Usijali kaka, maisha co kupanda na kushuka, maisha ni MABADILIKO. from one stage to another, ushajiweza kiuchumi wekeza katika mengne.

  7. David Bupilipili says

    Mimi mwenyewe unanigusa kinouma hadi nmeamua kutafuta mashairi yake

  8. Michael says

    keep your focus and always think postive

  9. Paul Fussi says

    Yeah! jua kuwa kuna maisha baada ya hapo kiuchumi upo vizur wekeza kweny mambo mengin BABA LATILAALA kama kilimo migodini au?

  10. ali masanyika says

    Your Comment
    Only God! knows.Time will tell.

  11. linah swai says

    daaa pole sna jua kwamba cku azifanan kupata na kukosa yote maisaha

  12. Deus silvan says

    Hakuna aijuae keshoyake kaka cha msingi mung amekupa afya,akili na nguvu tumia kipaj chako mung amekup nafas.

Leave A Reply