The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE VIDEO: Kwa Mara ya Kwanza… Diamond Amfungukia Harmorapa, Kolabo ya Harmonize na Harmorapa…!

EXCLUSIVE Stori ikufikie popote unapoifuatilia tovuti ya Global Publishers na Global TV Online ni kuhusu staa wa Bongo Fleva kutoka Wasafi (WCB), Diamond Platinumz kumzungumzia kwa mara ya kwanza msanii anaetikisa kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa, si mwingine ni Harmorapa anayefananishwa na msanii kutoka lebo ya WCB, Harmonize.

Harmorapa ambaye juzi aliachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha mkogwe wa Bongo Fleva, Juma Nature, “Kiboko Ya Mabishoo” amekuwa maarufu huku ghafla na kuwashangaza mastaa wengi na wadau wa muziki hapa Bongo.

Global TV Online imefanikiwa kumnasa Diamond na kufanya naye Exclusive Interview ili azungumze chochote kuhusu kumfahamu Harmorapa, kazi, kipaji chake cha muziki pamoja na mambo mengine.

Haya ni maneno ya Diamond Platinumz kuhusu Harmorapa

“Huwezi kujua Harmorapa ametokea wapi, pengine amesota sana mpaka kufikia hapo, mimi nimtie moyo afanye kazi nzuri zaidi ambayo itamfanya aje kuwa msanii mkubwa na kujipatia riziki kupitia kipaji chake…..”

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita, dancer wa Diamond ambaye ni mpenzi wa muigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, Mose Iyobo alimuita Harmora kuwa ni nyani hali iliyosababisha minong’ono mingi kwenye mitandao ya kijamii.

Mbali na hayo, Diamond aliulizwa kuhusu kolabo ya Harmonize na Harmorapa, ambapo aljibu anamuachia Harmonize aamue….!

MSIKIE DIAMOND MWENYEWE AKIFUNGUKA KUHUSU HARMORAPA

Comments are closed.