The House of Favourite Newspapers

Diamond afungukia kuchelewa kuchukua tuzo za MTV

0

hhj2Staa anayekimbiza kunako muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Musa mateja
STAA anayekimbiza kunako muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefungukia sababu zilizomfanya kuchelewa kuchukua tuzo za MTV Europe (EMA) na kuchukua Desemba mwaka huu ni kuwa hazikuwa halisi.

Akizungumza na Amani, Diamond aliyepata tuzo katika vipengele vya Msanii Bora Afrika pamoja na Msanii Bora kutoka Afrika/India alisema kuwa tuzo hizo walitangazwa kushinda lakini hawakukabidhiwa zaidi ya kupewa ruhusa ya kupiga nazo picha tu kisha zikarudishwa kutengenezwa upya.

“Hazikuwa silva orijino kwa hiyo sababu kubwa iliyofanya tusichukue siku ileile tulipoishinda ni kwamba walizirudisha kuzitengeneza upya na kuwa silva orijino,” alisema Diamond.

Tuzo zilifanyika rasmi Oktoba mwaka huu ambapo Diamond alifanikiwa kuwapita mastaa kibao wa muziki Afrika kama vile AKA (Afrika Kusini), Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria) na kuingia katika hatua nyingine ambapo alichuana na mwanamuziki, Priyanka Chopra kutoka India na kufanikiwa kuibuka kidedea.

Diamond kwa sasa anabamba na Wimbo wa Utanipenda ambao video yake imekuwa gumzo kila kona kutokana na mandhari na mashairi yaliyotumika. Staa huyo pia anatamba na nyimbo kibao kama vile Nana, Nasema Nawe, Mdogomdogo na nyingine nyingi.

Kwa mara ya kwanza, Diamond anatarajia kupiga Wimbo wa Utanipenda live kwa kutumia vyombo Krismasi hii (Desemba 25) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem.

Akizungumzia shoo hiyo, meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mashabiki wa burudani huu ni wakati wao na kwamba Dar Live imewaandalia burudani kabambe ukiachana na Diamond.

“Tutakuwa na Msagasumu ambaye wengi wanamtambua kama mkali wa Singeli ambapo siku hiyo atadondosha nyimbo zake zote kali kama vile Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Naipenda Simba na nyingine nyingi.

“Mbali na hiyo pia mashabiki wataburudika na kundi linalotamba Afrika Mashariki katika miondoko ya sarakasi na kucheza, Wakali Dancers ambapo nao siku hiyo watafanya maajabu kwa kucheza kwa staili za kila aina nyimbo kali zinazotikisa ndani na nje ya nchi,” alisema Mbizo.

Leave A Reply