The House of Favourite Newspapers

Diamond Akiwasha Mbaya Tuzo za Grammy

0

SUPASTAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameingia kwenye rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye mradi maalumu uitwao ‘Global Spin’ ulioandaliwa na waandaaji wa tuzo kubwa duniani za Grammy ambapo msanii huyo ametumbuiza kupitia Virtual concert iliyorushwa Januari 7, 2022.

 

Global Spin ni sehemu ya hafla maalumu iliyoanzishwa mnamo mwaka 2021, kwa lengo la kuutangaza muziki wa Afro Beat, K pop, pamoja na muziki wa Latin ili kuusogeza kwenye ramani ya muziki wa dunia.

 

Kwenye onesho hilo Diamond Platnumz ametumbuiza wimbo wake mpya ‘Gidi ambao bado hajautoa rasmi, huku miongoni mwa vivutio vikubwa ikiwa ni mpangilio wa namna wahusika wote kwenye onesho hilo walivyokaa na kunakshiwa na mandhari nzuri aliyoiandaa.

Leave A Reply